Raphael L Emmy Ft Goodluck Gozbert -sina hasara (Official Video) New 2019

Ni baada ya kutafakari kwa kina jinsi ambavyo watu hutoa muda wao mwingi kwajili ya kumtumikia Mungu kupitia vipawa na karama mbali mbali alizowapatia.
Imejengeka dhana kuwa mtu akitumia muda mwingi sana katika kumtumikia Mungu anaonekana kama anapoteza muda na hakuna faida yoyote katika hilo. La hasha….!!!

Nimeshuhudia kwa macho yangu namna ambavyo Mungu amekuwa akinivusha vikwazo tena kwa hatua zenye mpangilio maalumu kutoka chini mpaka iliko ahadi yake.
Nimejua kuwa kumbe SINA HASARA na wala siko kupoteza muda najua aliloniahidi Mungu liko mbele yangu nalo ni KUBWA, REFU na PANA lenye viwango vya juu mno.

Ungana nami katika tafakari hii useme kwa kinywa chako kuwa huna HASARA ili umkumbushe Mungu ahadi aliyoiahidi kwako na najua itakapo timia hautabaki kama ulivyo sasa. Ameeeen

Lyrics

SINA HASARA kwako ×2

Oooh
Ee Bwana Yesu sijawahi juta kwako nina raha moyoni
Hatua zangu zitanifikisha ng’ambo kwakuwa uko na mimi

Mmmm
Wewe si sawa na mwanadamu jinsi unavyotenda
Waniongoza njia zangu kama kama unavopenda
Unasamehe dhambi zangu, umejaa rehema
Na nikichoka wanipa nguvu nasimama.

SINA HASARA kwako ×4

Kuna wakati nilijiuliza kwako wanapata nini
Sikufikiri ndani ya pendo lako kuna tumaini
Nami nakili nilipokuwa huko sikuwa na amani
Nikabadili njia na kurudi kwako nikae uweponi

Ninaijua kesho yangu sababu namjua mwenye kesho
– na kwakuwa unalo kusudi, kusudi takatifu umeliweka kwangu
Sitapungukiwa kitu sababu Mali nyingi ziko kwako
– sisumbuliwi na utajiri vyote navipata toka kwako

Umenifanya wa pekee, umeniondolea hofu
Kila siku ni sherehe umenifanya niwe juu
Kuwa nawe ni starehe, tabasamu kila siku
Leo hata milele nitakuita Mungu wangu.

Wewe si sawa na wanadamu jinsi wanavyotenda
Waniongoza njia zangu kama kama unavopenda
Unasamehe dhambi zangu, umejaa rehema
Na nikichoka wanipa nguvu nasimama

SINA HASARA kwako ×4


Recommended Videos